• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia laki 1.1 wa Syria waondoka eneo la Ghouta Mashariki

    (GMT+08:00) 2018-03-26 09:09:20

    Shirika la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, raia zaidi ya laki 1 wameondoka eneo la Ghouta Mashariki, mji mkuu wa Damascus, tangu mapema mwezi huu.

    Jeshi la Syria limehakikisha kuhama huko na idadi ya raia waliohamishwa inaongezeka kila siku tangu zoezi hilo lianze katikati ya Mwezi Machi.

    Shirika la haki za kibinadamu nchini Syria linakadiria kuwa idadi ya raia walioondoka kutoka sehemu hiyo itafikia laki 1.4.

    Uhamiaji huo unaendelea huku wapiganaji na familia zao wakiondoka kutoka mji wa Ghouta.

    Shirika hilo pia limesema jeshi la Syria limetwaa asilimia 90 ya sehemu ya Ghouta Mashariki ikiwa sehemu ya operesheni ya kijeshi iliyoanza mwezi uliopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako