• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yakamailisha hatua za mwisho za maandalizi ya uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2018-03-26 09:17:11

    Mamlaka ya Misri iko kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya uchaguzi wa rais utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia leo, huku rais wa sasa Abdel-Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.

    Waziri wa maendeleo wa Misri Bw. Abu Bakr al-Gendy ametoa taarifa akisema maandalizi yote yamekamilika kwa kushirikiana na serikali za majimbo na mashirika yanayofuatilia mchakto wa uchaguzi huo.

    Amesema Misri imemaliza kuandaa vituo vyote vya kupigia kura na kutoa njia zote za kupokea na kukaribisha wananchi kupiga kura.

    Misri ina wapiga kura halali zaidi milioni 59 kati ya watu milioni 104. Wiki iliyopita, Misri ilikamilisha mchakato wa upigaji kura nje ya nchi katika nchi 124 kote duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako