• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu, Mashindano ya Kenya 2018: Rais Uhuru Kenyatta ampongeza bingwa mpya wa mashindano

    (GMT+08:00) 2018-03-26 10:06:06

    Lorenzo Gagli wa Italia ameshinda ubingwa wa mashindano ya Golf ya Kenya yaliyomalizika jana katika viwanja vya Muthaiga mjini Nairobi, kwa kuwashinda wenzake zaidi ya mia moja walioshiriki mashindano hayo wakiwemo wa kulipwa na wachezaji wa ridhaa.

    Kutokana na ushindani mkubwa uliojitokeza katika siku ya mwisho, iliwalazimu Gagli na Jens Fahrbrings wa Sweden kushindanishwa baada ya kuwa na alama zinazoshabihiana katika matokeo ya mwisho, ambapo makosa madogo yaliyofanywa na Jens yalimnufaisha Gagli na kunyakua ushindi.

    Mchezo huo wa fainali ya wawili ulikuwa kivutio kwa watu wengi, hata ukahudhuriwa na mashabiki wengi wakiwemo Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Raila Odinga.

    Kwa ushindi huo Gagli alijinyakulia tuzo na fedha taslimu yenye thamani ya Yuro 80,000 sawa na shilingi milioni 10 za Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako