• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taekwondo: Timu ya Rwanda yatamba kutetea ubingwa wake itakaposhiriki mashindano ya mwaka huu nchini Morocco

  (GMT+08:00) 2018-03-26 10:07:11

  Timu ya taifa ya Rwanda ya mchezo wa Taekwondo imetamba kushinda katika michuano ya Afrika itakayofanyika kuanzia Machi 28 hadi April 1 mjini Agadir nchini Morocco.

  Timu hiyo inayojumuisha wachezaji 14 wanawake na wanaume, wanaoshiriki vipengele vyote vya mchezo huo, wakiwemo 6 wanaoshiriki taekwondo maalum kwa watu wenye ulemavu (Para-Taekwondo).

  Katika mashindano kama hayo mwaka jana, Rwanda wakiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza na wakiwa wenyeji walishinda ubingwa wa jumla kwa kujinyakulia medali 2 za dhahabu, 3 za fedha na moja ya shaba, hivyo kutokana na maandalizi makali waliyofanya wanaamini kuwa watatetea ubingwa huo.

  Katika mashindano ya mwaka huu, Rwanda wanatarajia kukumbana na ushindani mkali kutoka kwa timu za Misri, Algeria, Tunisia, Gabon na wenyeji Morocco.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako