• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Wanawake: Timu ya Taifa ya Kenya yaifunga Zambia kwa magoli 3-0 katika mchezo wa kirafiki

    (GMT+08:00) 2018-03-26 10:07:31

    Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ya Kenya (Harambe Starlets) imeifunga timu ya Zambia She-Polopolo kwa magoli 3-0 katika mechi ya kirafiki iliyofanyika jana mjini Kitwe nchini Zambia.

    Magoli ya Kenya yalifungwa na Mwanahalima Adam aliyefunga la kwanza dakika ya 18, na mengine mawili yakifungwa na mchezaji mzoefu katika timu hiyo Corazon Acquino kunako dakika za 78 na 83.

    Kwa mujibu wa kocha mkuu Richard Kanyi, mechi dhidi ya Zambia ilikuwa maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kombe la mataifa ya Afrika 2018, dhidi ya majirani zao Uganda mwezi ujao.

    Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu yanafanyika mwezi Novemba nchini Ghana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako