• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Magari ya Mwendokasi: Vettel atetea ushindi wa mashindano ya kwanza nchini Australia

    (GMT+08:00) 2018-03-26 10:07:50

    Sebastian Vettel wa Ujerumani ameshinda taji la mbio za kwanza za mashindano ya magari ya mwendokasi maarufu kama Langalanga, zilizofanyika jana mjini Melbourne nchini Australia.

    Katika mzunguko wa mwisho katika sakiti hiyo yenye urefu wa kilomita 5.4 alifanikiwa kuwapita madereva wawili waliokuwa mbele yake, Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes aliyeshika nafasi ya pili na dereva mwenzake wa timu ya Ferrari Kimi Raikkonnen aliyeshika nafasi ya tatu.

    Kwa ushindi huu Vettel amefanikiwa kutetea taji hilo ambalo hata msimu uliopita alifanikiwa kulitwaa.

    Kukamilika kwa mbio hizi za kwanza kunawapa madereva muda wa kujiandaa na mbio za Bahrain zitakazofanyika April 8 mjini Sakhir.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako