• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 53 wafariki katika ajali ya moto iliyotokea kwenye jengo la maduka nchini Russia

    (GMT+08:00) 2018-03-26 16:44:11

    Watu 53 wamefariki kwenye ajali ya moto iliyotokea jana kwenye jengo la maduka mjini Kemerovo nchini Russia.

    Taarifa iliyotolewa na idara kuu ya hali za dharura ya jimbo la Kemerovo imesema, kazi za uokoaji zilizoendelea kwa saa 14 mfululizo, zimesimama kutokana na moshi wingi na joto kali. Awali, idara hiyo ilisema, bado kuna watu 64, wakiwemo watoto 41 ambao hawajulikani walipo.

    Hivi sasa moto huo umezimwa na watu wanne wamekamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako