• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema ziara ya Wang Yi itaonesha umaalum wa uhusiano kati ya China na Russia

    (GMT+08:00) 2018-03-26 18:05:39

    Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi kesho atafanya ziara nchini Russia.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, ziara hiyo imeonesha kiwango cha juu na umaalum wa uhusiano kati ya China na Russia. Amesema, uhusiano kati ya China na Russia una fursa mpya ya maendeleo baada ya rais Vladimir Putin kuchaguliwa tena kuiongoza Russia.

    Bw. Wang Yi atakutana na viongozi wa Russia na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergej Lavrov na kubadilishana maoni kuhusu mpango wa mawasiliano ya viongzi wa pande mbili wa mwaka huu na kuhimiza ushirikiano katika sekta muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako