• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Marekani wa kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China unalenga kushusha kasi ya maendeleo ya sekta zenye nguvu

    (GMT+08:00) 2018-03-26 18:08:29

    Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Dunia iliyo chini ya Baraza la Serikali la China Ding Yifan amesema, Marekani kuongeza ushuru wa dola za kimarekani bilioni 60 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China sio hatua inayofaa na nchi hiyo itaumia yenyewe.

    Bw. Ding amesema pengo la biashara kati ya Marekani na China halimaanishi kuwa Marekani inapata hasara kwani inaweza kutumia fedha kupata kitu inachotaka, lakini kama kitu hicho kinatengenezwa nchini, bei itakuwa juu. Amesema bidhaa zitakazoongezewa ushuru kwa mujibu wa mpango huo ni pamoja na mashine za matibabu, dawa, rasilimali mpya, mashine za kilimo na bidhaa za usafiri wa anga, sekta ambazo zote zimejumuishwa kwenye "Mpango wa Kutengenezwa China wa Mwaka 2025". Anasema, (Sauti 4) "Baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa Marekani wanaogopa kuwa kama China itapata maendeleo makubwa katika sekta hizo, nguvu bora za Marekani na nchi za magharibi hazitakuwepo na bidhaa zao zitakosa ushindani."

    Baada ya rais Trump kusaini kumbukumbu ya kuongeza ushuru, Wizara ya Biashara ya China imeandaa orodha ya bidhaa za Marekani zitakazoongezewa ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako