• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema ugaidi hautavuruga juhudi za kuleta amani Somalia

    (GMT+08:00) 2018-03-26 18:15:35

    Tume ya Msaada ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM imelaani shambulizi la mabomu yaliyotegwa kwenye gari mjini Mogadishu lililofanyika jana na kusababisha vifo vya watu watano, na kusema kuongezeka kwa vitendo vya ugaidi hakutavuruga juhudi za kuleta amani nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo pia imetoa pole kwa wafiwa katika shambulizi hilo. Tukio hilo limetokea baada ya gari lililotegwa mabomu kulipuka kwenye kituo muhimu cha ukaguzi mjini Mogadishu.

    Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako