• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima waitaka serikali kutoa mbolea kufanikisha shughuli za upanzi

    (GMT+08:00) 2018-03-26 19:25:23

    Wakulima wa Kenya wameiomba serikali ya kitaifa kutoa mbolea ya kutosha ili kufanikisha shughuli za upanzi msimu huu ambao taifa linashuhudia mvua.

    Upungufu wa mbolea nchini hasa maeneo yanayokuza mahindi kwa wingi umetajwa kama kizingiti cha upanzi wa mapema. Bi Mary Ndzomo ambaye ni afisa wa kilimo kaunti ya Trans-Nzoia anasema wakulima wengi wamesitisha upanzi wa mahindi kwa sababu ya upungufu wa mbolea.Ameongeza kuwa miaka ya awali Trans Nzoia imekuwa ikivuna wastani wa magunia milioni 7 kila mwaka lakini mwaka 2017 kaunti hiyo ilivuna magunia milioni 4.8 kwa sababu ya upungufu wa mbolea na kero la wadudu aina viwavijeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako