• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuwaita kuipa Tanzania mkopo wa masharti nafuu

    (GMT+08:00) 2018-03-26 19:26:35

    Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa nchi hiyo imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 207.3 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma yenye urefu wa kilometa 257.

    Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Kuwait nchini humo Bw Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Daktari Philip Mpango.

    Balozi Al-Najem amesema mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.

    Ameahidi kuwa nchi hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili ikuze uchumi na maisha ya watu wake.

    Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, maji na afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako