• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM alaani kundi la Houthi kurusha makombora nchini Saudi Arabia

    (GMT+08:00) 2018-03-27 08:52:34

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amelilaani kundi la Houthi kwa kurusha makombora nchini Saudi Arabia jumapili iliyopita. Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema kupitia taarifa kuwa Bw. Guterres anazitaka pande zinazopambana nchini Yemen kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria ya ubinadamu ya kimataifa, kulinda usalama wa raia na miundombinu ya kiraia, na pia ametoa wito kwa pande mbalimbali kujizuia na kusisitiza kuwa njia ya kijeshi kamwe sio utatuzi, na mgogoro wa Yemen unatakiwa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo shirikishi kati ya pande husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako