• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN: Upanuzi wa makazi haramu ya wayahudi watishia ufumbuzi wa nchi mbili

    (GMT+08:00) 2018-03-27 08:53:12

    Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa mchakato wa amani wa Mashariki ya kati Bw. Nickolay Mladenov amesema upanuzi wa makazi haramu ya wayahudi na shughuli husika zinaendelea kutishia uwezekano wa kufanikisha ufumbuzi wa nchi mbili, na kuhujumu mustakbali wa kutimiza amani kwenye eneo la Mashariki ya kati. Bw. Mladenov amesema azimio Nambari 2334 la Umoja wa mataifa linaitaka Israel kusitisha mara moja na kikamilifu shughuli zote zinazohusu makazi kwenye ardhi ya Palestina inayokalia, ikiwemo Jerusalem mashariki, lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako