• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa waimarisha juhudi za kibinadamu kuhusu Syria

    (GMT+08:00) 2018-03-27 09:17:00

    Umoja wa mataifa unaimarisha juhudi zake kushughulikia mahitaji ya watu walioathiriwa na mapambano yanayoendelea katika eneo la Afrin kaskazini mashariki mwa Syria.

    Naibu msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema mapambano yanayoendelea katika eneo hilo yamesababisha kutokea kwa vifo na majeruhi, uharibifu wa miundombinu ya kiraia, na kufanya watu wengi kupoteza makazi.

    Amesema msafara wa magari wa Umoja wa mataifa na Shirika Hilari nyekundu la Syria kuelekea katika mji wa Tal Refaat ulipeleka chakula na vifaa vya afya kwa ajili ya watu elfu 50 waliokimbia makazi yao kutoka eneo la Afrin.

    Inakadiriwa kuwa watu laki 1.83 wakiwa ni pamoja na wanawake na watoto, wamepoteza makazi yao, na wingi wao umekuwa ni mzigo mkubwa kwa watu wanaowapokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako