• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa wapokea taarifa ya Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia katika umoja wa mataifa

    (GMT+08:00) 2018-03-27 09:17:19

    Umoja wa mataifa umepotea taarifa ya uamuzi wa Marekani kuwafukuza wanadiplomasia 12 wa Russia kwenye ujumbe wake katika umoja wa mataifa. Msemaji wa umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amethibitisha kuwa ujumbe wa Marekani kwenye umoja huo umewasilisha taarifa ya uamuzi wa kuwafukuza baadhi ya wawakilishi wa Russia, unaowataka waondoke Marekani.

    Uamuzi wa Marekani unatajwa kuwa ni kuonyesha uungaji mkono kwa Uingereza, ambayo inadai kuwa Russia inahusika na shambulizi la sumu lililotokea Machi 4 nchini Uingereza dhidi jasusi wa zamani wa Russia. Pamoja na wanadiplomasia hao 12, Marekani imewafukuza wanadiplomasia 60 kwa jumla na kufunga ubalozi mdogo wa Russia mjini Seattle. Uingereza pia imewafukuza wanadiplomasia 23 wa Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako