• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezo ya Jumuiya ya Madola 2018: Kundi la Kwanza la wanamichezo lawasili nchini Australia

  (GMT+08:00) 2018-03-27 09:53:11

  Kundi la kwanza la wanamichezo kutoka Kenya watakaoshiriki mashindano ya jumuiya ya madola, limewasili salama jana katika mji wa Gold Coast nchini Australia.

  Akitangaza wanamichezo hao waliotangulia, kiongozi wa timu ya Kenya kwenye mashindano hayo Bw. Barnabas Korir, amesema wamo waendesha baiskeli za mashindano, wanamasumbwi, wanyanyua vitu vizito pamoja na timu ya madaktari.

  Kiongozi huyo amesema fungu hilo la kwanza limelazimika kuwasili mapema kwa kuwa michezo yake inafanyika katika siku za mwanzo.

  Kundi lingine la timu ya Kenya linatarajiwa kuwasili leo, na kundi la mwisho ambalo litajumuyisha wanariadha, timu ya raga na baadhi ya viongozi litaondoka mwishoni mwa juma hili kwa kuwa michezo yao ipo katika tarehe za mwisho za mashindano hayo yanayoanza rasmi April 4 na kumalizika April 15.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako