• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu Rwanda: Rayon Sport wafanikiwa kuongoza katika mzunguko wa kwanza wa msimu, kuzawadiwa milioni 10 na wadhamini

    (GMT+08:00) 2018-03-27 09:54:05

    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya nchini Rwanda Rayon Sport wamefanikiwa kukamata usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 30 kufuatia ushindi wa magoli 3-2 iliopata jana kwenye mechi dhidi ya timu ya Sunrise FC.

    Goli la ushindi la Rayon lilifungwa na Faustin Usengimana katika dakika ya 70, na kuifanya timu hiyo imalize mzunguko wa kwanza kwenye msimu huu ikiwa kileleni mwa ligi.

    Katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo timu zote zilikamatana kwa sare ya magoli 2-2, ambapo Rayon ilitangulia kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Bonfils Bimenyimana.

    Alex Ortomal na Osee Iyabivuze walisawazisha magoli yote hayo katika kipindi cha kwanza.

    Lakini kutokana na kuongoza ligi katika nusu ya msimu Rayon watajipatia donge nono la Faranga za Rwanda milioni 10 kutoka kwa wadhamini.

    Mahasimu wa Rayon, APR wenye pointi 25 wanacheza leo mjini Byumba dhidi ya wenyeji wao Gicumbi FC

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako