• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitaki, lakini haiogopi vita ya kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-03-27 10:09:25

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Zheng Zeguang amesema, hatua ya Marekani ya kutangaza kwa upande mmoja matokeo ya uchunguzi 301 dhidi ya China, hailingani na kanuni za WTO, na nia ya ushirikiano kati ya sekta za viwanda na biashara za nchi hizo mbili. Amesisitiza kuwa China haitaki, lakini haiogopi vita ya kibiashara.

    Bw. Zheng Zeguang amesema hayo alipotoa hotuba ya "Diplomasia yenye umaalumu wa China katika zama mpya" katika Mkutano wa 19 wa Baraza la ngazi ya juu ya maendeleo ya China.

    Bw. Zheng amesisitiza kuwa China ina nia thabiti na imejiandaa kujibu hatua hiyo ya Marekani, ili kulinda maslahi ya nchi. Anaitaka Marekani itulie, na kutafuta ufumbuzi mwafaka wa suala hilo kwa kufuata msingi wa kuheshimiana na kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako