• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China azungumza na wajasiriamali wa makampuni maarufu duniani ikiwemo Apple, Hitachi, na Google.

  (GMT+08:00) 2018-03-27 15:35:06

  Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang amesema ukubwa wa leo wa biashara kati ya China na Marekani umepatikana kutokana na nguvu ya soko na kanuni za biashara, na msingi wa kusaidiana na kunufaishana. Kukosekana kwa uwiano kwenye biashara kati ya pande hizo kunapaswa kutatuliwa kwa kuongeza zaidi ukubwa huo, na tofauti zinapaswa kutatuliwa kwa kupitia mazungumzo na mashauriano.

  Waziri mkuu wa China Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na wageni wanaoshiriki kwenye Kongamano la Ngazi ya Juu la Maendeleo la China la mwaka wa 2018, ambapo amejibu maswali yaliyotolewa na wajumbe kutoka makampuni ya Apple, Hitachi, Starr, na Google, pamoja na Chuo Kikuu cha Cambridge na kampuni ya Qualcomm. Alipojibu swali la mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya uwekezaji ya Starr ya Marekani Maurice Greenberg kuhusu mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani, waziri mkuu Bw. Li Keqiang amesema hakuna mshindi kwenye vita ya biashara.

  "Jumuiya ya kimataifa inapaswa kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi, na kupinga moja kwa moja sera ya kujilinda na ya upande mmoja. Haitakuwa na mshindi kwenye vita ya biashara. China na Marekani zinapaswa kuwa na msimamo wa kuangalia hali halisi na tahadhari katika kukabiliana na hali ya kukosekana kwa uwiano kwenye biashara kati ya pande hizo, na kuongeza ukubwa wa biashara ili kuhimiza uwiano. Tofauti zinapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo na mashauriano. La sivyo, nchi zote mbili na hata dunia nzima itapata hasara."

  Bw. Li amesema kufungua mlango ni sera ya msingi ya taifa la China, na China itaimarisha zaidi sera hiyo.

  "Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, na China itafungua zaidi mlango wake, jambo ambalo linalingana na maslahi ya maendeleo ya China, na pia kusaidia kulinda biashara huria na maendeleo mazuri ya dunia. Tunapenda kujifunza teknolojia ya kisasa na uzoefu mzuri wa usimamizi wa nchi za nje, kupanua ushirikiano kwenye sekta za bidhaa, ujuzi, teknolojia na huduma."

  Hivi sasa, China inatekeleza mkakati wa "Made in China 2025" ambao ni mpango wa utekelezaji wa miaka kumi ya kwanza katika mkakati wa kuijenga China iwe taifa lenye nguvu katika utengenezaji. Bw. Li amesema China inakaribisha makampuni yenye ushindani ya nchi za nje kuja China na kunufaika na fursa za maendeleo yaliyopo hapa China.

  "'Made in China China 2025' inatekelezwa kwenye mazingira ya uwazi, na makampuni ya ndani ya nje ya nchi yako sawa katika kushiriki kwenye mpango huo. Hatutalazimisha makampuni ya nchi za nje kuhamisha teknolojia zao, na China itaongeza nguvu ya kulinda haki miliki, na kupambana na vitendo vya kukiuka hakimiliki."

  Mwakilishi wa washiriki ambaye ni ofisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Apple Tim Cook amesema, anaamini kuwa maendeleo ya China yatatoa fursa kwa maendeleo kwa dunia nzima, na kampuni zao zinapenda kushiriki kwenye mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango ya China na kutimiza kusaidiana na kunufaishana.

  "Natoa shukrani kwa waziri mkuu Bw. Li Keqiang kwa kukaa nasi kufanya majadiliano ya dhati. Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango. Mimi na wajasiriamali wote wa makampuni ya nchi mbalimbali tunaoshiriki kwenye mkutano huu, tunatarajia kuwa China itaimarisha zaidi sera ya mageuzi na ufunguaji mlango."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako