• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa umeme lataka mafundi feki wakamatwe

    (GMT+08:00) 2018-03-27 19:08:20

    Shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa umeme nchini Kenya limeitaka Tume ya Kudhibiti Nishati nchini (ERC) kufanya uchunguzi ili kuwanasa mafundi feki wa umeme nchini.

    Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Francis Kimani alilalama kuwa mafundi feki wa umeme ndio chanzo cha mikasa ya moto ambayo imekuwa ikiteketeza majumba ya makazi.

    Kimani alisema kunapaswa kuwa na ushirikiano wa kuwatimua mafundi wasio na leseni ambao wamewapokonya kazi zao.

    Aidha Mwenyekiti huyo alilalama kuwa kumekuwa na ongezeko la uuzaji wa nyaya feki za umeme ambazo zimekuwa zikiuzwa na wafanyabiashara walaghai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako