• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano yawahamasisha wanawake kuchangamkia fursa za ujenzi na barabara

    (GMT+08:00) 2018-03-27 19:09:01

    Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imetaka wanawake walio katika sekta ya uhandisi wenye fursa za kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na matengenezo ya barabara kuhamasisha wenzao katika kazi za miradi hiyo.

    Hatua hiyo imeelezwa itasaidia kuongeza ushirikishwaji wa wanawake katika sekta hiyo ili kufikia lengo la kuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume ifikapo mwaka 2025.

    Mkuu wa Chuo cha Ujenzi Morogoro Melkzedeck Mlyapatali amewataka wahandisi wa kike kuwahamasisha na kuwaelimisha wanawake katika maeneo yao ya kazi kuchamngamkia fursa hizo.

    Mlyapatali alikuwa akizungumza wakati wa ufungaji wa semina elekezi kwa waratibu wa mikoa wa ushirikishwaji wa wanawake katika akzi za barabara kutoka ofisi za wakala wa barabara (Tanroads) kutoka mikoa yote ya Tanzania bara.

    Mratibu wa kitengo cha ushirikishwaji wa wanawake katika akzi za barabarani kutoka Wizarani,Mhandisi Rehema Myeya alihimiza waratibu walioshiriki semina hiyo kuhakikisha kuwa wanawake watakaopata kazi za ujenzi au matengenezo ya barabara wazifanye katika viwango vinavyokubalika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako