• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China aitaka Marekani kutumia busara na ufanisi na kushirikiana na China ili kutatua mvutano wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-03-27 21:19:11

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na ujumbe wa wabunge wa Marekani unaoongozwa na seneta Bw. Steve Daines hapa Beijing, na kusema China inaitaka Marekani kuchukua msimamo wenye busara na kuangalia hali halisi, na kushirikiana nayo ili kutatua mvutano wa kibiashara.

    Bw. Li amesema, vita vya kibiashara haviwezi kutatua tatizo, na China itafanya juhudi ya kutatua mvutano huo kwa mazungumzo, huku ikifanya maandalizi ya kutosha kukabiliana na vita hivyo.

    Kwa upande wake, Bw. Daines amesema, uhusiano kati ya Marekani na China ni moja kati ya mahusiano muhimu zaidi ya pande mbili, na kwamba nchi hizo hazina sababu za kuwa na mvutano. Pia amesema Bunge la Marekani linapenda kutatua mvutano huo kwa njia ya kunufaishana, ili kuufanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelea kuwanufasha watu wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako