• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw. Xi Jinping na Bw. Kim Jong-un wafanya mazungumzo

  (GMT+08:00) 2018-03-28 08:37:40

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un amefanya ziara isiyo rasmi nchini China kuanzia tarehe 25 hadi 28 mwezi huu nchini China kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China.

  Katika ziara hiyo, rais Xi Jinping amefanya mazungumzo na Bw. Kim Jong-un katika Jumba la mikutano ya umma la Beijing. Kwenye mazungumzo yao, rais Xi amemkaribisha Bw. Kim Jong-un nchini China, na kusema ziara hiyo inayofanyika katika wakati maalumu ina umuhimu mkubwa, na imeonesha kuwa Bw. Kim Jong-un na kamati kuu ya chama cha Leba cha Korea Kaskazini wanatilia maanani sana uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

  Kwa upande wake Bw. Kim Jong-un amesema anapaswa kuja China kutoa pongezi uso kwa uso kwa rais Xi Jinping kuchaguliwa tena kuwa rais wa China na mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya kamati kuu ya chama cha CPC. Amesema hivi sasa hali ya peninsula ya Korea imepiga hatua haraka na mabadiliko mengi muhimu yametokea, na hivyo inambidi aripoti kwa rais Xi Jinping kuhusu mambo yanayotokea kwenye peninsula ya Korea.

  Rais Xi amesema urafiki wa jadi kati ya China na Korea kaskazini ni urithi muhimu kwa pande zote mbili, na katika miaka mingi iliyopita, China na Korea Kaskazini na vyama vyao vimeungana mkono na kushirikiana, na kutoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya ujamaa. Amesema yeye mwenyewe na Bw. Kim Jong-un ambao wote wameshuhudia maendeleo ya uhusiano wa nchi mbili, wamesisitiza mara nyingi kuwa wataenzi urafiki wa nchi mbili kizazi baada ya kizazi na kuuendeleza zaidi, na hili ni chaguo la kimkakati na pia ni chaguo pekee lililo sahihi lililoamuliwa na pande zote mbili kutokana historia na hali ya sasa, kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa ya kikanda na ya kimataifa, pamoja na maendeleo ya uhusiano kati ya China na Korea Kaskazini.

  Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa chama na serikali ya China inatilia maanani uhusiano na ushirikiano kati ya China na Korea Kaskazini, na kulinda, kuimarisha na kukuza uhusiano huo ni mkakati thabiti wa chama na serikali ya China. Amesema China inapenda kushirikiana na makomredi wa Korea Kaskazini, katika kusukuma mbele uhusiano wa China na Korea Kaskazini uendelee kupiga hatua kwa utulivu, ili kuwanufaishana wananchi wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya kikanda. Rais Xi amesema kwanza ni kuendelea kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili, ambayo siku zote yanafanya kazi muhimu ya uongozi na uhimizaji kwenye maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili. Rais Xi amesema katika hali mpya anapenda kudumisha mawasiliano ya mara kwa mara na Bw. Kim Jong-un kwa njia za kutembeleana, kutumiana wajumbe na kuwasiliana kwa barua. Pili ni kutumia barabara mbinu ya jadi ya mawasiliano ya kimkakati. Rais Xi amesema vyama vya China na Korea kaskazini vimekuwa na desturi ya kubadilishana maoni kuhusu masuala muhimu, hivyo pande hizo mbili zinapaswa kutumia vizuri fursa muhimu za mawasiliano kati vyama, katika kuhimiza ushirikiano na mawasiliano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali, ili kuimarisha hali ya kuaminiana. Tatu ni kuhimiza maendeleo kwa njia ya amani. Hivi sasa ujamaa mwenye umaalumu wa China umeingia kwenye zama mpya, huku ujenzi wa ujamaa nchini Korea Kaskazini pia ukiingia kwenye kipindi kipya. Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Korea Kaskazini, kuendana na wakati na kuinua juu bendera ya amani, maendeleo, ushirikiano na kunufaishana, ili kuendelea kuboresha maisha ya watu wa nchi mbili, na kutoa mchango chanya kwa ajili ya amani, utulivu na maendeleo ya kikanda. Nne ni kuimarisha uungaji mkono wa umma kwa urafiki kati ya China na Korea Kaskazini. Rais Xi amesema pande mbili zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya kiraia kati ya nchi mbili kwa njia mbalimbali, kuimarisha uungaji mkono wa umma kwa uhusiano wa kirafiki kati ya nchi mbili, haswa mawasiliano kati ya vijana wa nchi mbili, ili kurithi na kuenzi urafiki wa jadi kati ya China na Korea Kaskazini.

  Kim Jong Un amesema, Rais Xi Jinping ametoa maoni muhimu kuhusu Urafiki kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Korea na Jamhuri ya Watu wa China na kuendeleza uhusiano kati ya vyama viwili na wananchi wa nchi hizi mbili, maoni yake yamemtia moyo sana ni kumpa mwanga. Amesema viongozi waasisi wa nchi zao mbili walianzisha wenyewe na kulea kwa pamoja urafiki kati ya nchi zao, urafiki huo hautikisiki. Kurithi na kuendeleza urafiki kati ya Korea kaskazini na China katika hali mpya ni chaguo la kimkakati la upande wa Korea kaskazini, hili halitabadilika katika hali yoyote. Amesema kwenye hii ziara yake, ana matumaini ya kukutana na ndugu wa China, kuimarisha mawasiliano wa kimkakati, na kuzidisha urafiki wa jadi. Pia ana matumaini kuwa atapata fursa ya kutana mara kwa mara na Rais Xi katika siku za baadaye, kutumiana wajumbe maalumu, ama kuandikiana barua ili kudumisha mawasiliano ya karibu, na kuinua kiwango cha maendeleo ya uhusiano kati ya vyama viwili na nchi mbili kwa kupitia mkutano wa viongozi wakuu kwenye kiwango kipya.

  Kila upande wa pande hizi mbili uliufahamisha upande mwingine hali ya nchini mwake. Bw. Xi Jinping amesema, Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha kikomunisti cha China umetoa mpango kamambe wa kufanya ujenzi kwa pande zote nchi yenye nguvu ya kisasa ya Ujamaa, kukamilisha ujenzi wa Jamii yenye maisha bora kwa pande zote ifikapo mwaka 2020, kutimiza kimsingi mambo ya kisasa ya nchi ya Ujamaa yanayopendeza na yaliyo ya usitawi, demokrasia, ustaarabu na masikilizano, ambapo wachina wote wataendelea kufanya juhudi kubwa bila kujali taabu kwa ajili ya kutimiza Ndoto ya China ya usitawishaji mkubwa wa Taifa la China. Amesema katika miaka ya karibuni, China imeona kiongozi mkuu Kim Jong Un amekiongoza chama cha Korea ya kaskazini na wananchi wake na kutoa hatua mfululizo zenye hamasa katika kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, na kupata mafanikio mengi. Tuna matumaini kuwa Korea ya kaskazini itakuwa na utulivu wa siasa, maendeleo ya uchumi na maisha bora ya wananchi, sisi tunakiunga mkono chama cha Korea ya kaskazini ambacho kiongozi wake ni Kim Jong Un kuwaongoza wananchi wa Korea kaskazini kusonga mbele siku hadi siku kwenye njia ya Ujamaa, na kuwaunga mkono ndugu wa Korea kaskazini kwa juhudi zao kubwa katika kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

  Kim Jong Un amesema, tokea Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China, Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambacho kiini chake ni Rais Xi Jinping imeonesha ujasiri mkubwa wa kisiasa na kubeba wajibu mkubwa, imetoa fikra mpya na wazo jipya tena kuvitekeleza kivitendo, hivyo imetatua matatizo mengi na mambo makubwa ambayo hayakushughulikiwa vizuri kwa muda mrefu, hayo yameonesha vya kutosha kuwa, msimamo wa chama tawala cha China ni msimamo sahihi unaolingana na hali halisi ya nchi ya China, na kutimiza uongozi wa pande zote wa chama hiki katika kazi mbalimbali. Hivi sasa chama pia kinaonngeza nguvu, kwa kupambana na vitendo vya kuonesha ujeuri, umangimeza, na ufisadi. Wameyatakia kwa dhati mafanikio makubwa mapya yapatikane nchini China katika ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote, na ujenzi wa nchi ya kisasa yenye nguvu ya Ujamaa.

  Viongozi wa pande mbili wamebadilishana maoni kwa kina kuhusu hali ya kimataifa na hali ya Peninsula ya Korea.

  Bw. Xi Jinping amedhihirisha kuwa, tokea mwaka huu uanze, mabadiliko yenye hamasa yametokea katika hali ya Peninsula ya Korea. Upande wa Korea ya kaskazini umefanya juhudi muhimu kwa ajili ya hayo, na China inapongeza juhudi zake. Kuhusu suala la Peninsula ya Korea, amesema China inashikilia kutimiza lengo la kuifanya peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na nyuklia, na kulinda amani na utulivu wa peninsula hiyo, na kupitia mazungumzo na mashauriano kutatua matatizo. Amezitaka pande mbalimbali ziunge mkono pande mbili za kaskazini na kusini za peninsula hiyo kuboresha uhusiano kati yao, na kufanya juhudi halisi kwa pamoja katika kusuluhisha na kuhimiza mazungumzo ya amani. Upande wa China unapenda kuendelea kufanya kazi ya kiujenzi katika suala la Peninsula, na kujiunga na pande mbalimbali husika ukiwemo upande wa Korea kaskazini katika kuhimiza kwa pamoja hali ya Peninsula ielekee kupunguza hali ya wasiwasi.

  Kim Jong Un amesema, hivi sasa hali ya Peninsula ya Korea imeanza kuondoa vizuizi. Amesema Korea Kaskazini imeanza kuchukua hatua za kupunguza hali ya wasiwasi, na kutoa pendekezo la kufanya mazungumzo ya amani. Kwa kufuata wosia wa Mwenyekiti Kim Il sung na katibu mkuu Kim Jong Il, tunajikita katika kutimiza lengo la kuifanya peninsula iwe sehemu isiyo na nyuklia, huu ni msimamo wetu ambao hautabadilika siku zote. Amesema Korea Kaskazini imedhamiria kuubadilisha uhusiano kati ya kaskazini na kusini uwe uhusiano wa maafikiano na ushirikiano, kufanya mkutano wa wakuu wa pande zetu mbili, na kupenda kufanya mazungumzo na Marekani, kujenga hali ya amani na utulivu, na kuchukua hatua za kipindi na hatua za pamoja kwa ajili ya kutimiza amani, hivyo suala la kuifanya peninsula ya Korea iwe sehemu isiyo na nyuklia litaweza kutatuliwa. Amesema katika mchakato huo, wana matumaini ya kufanya mawasiliano ya kimkakati na China, ili kulinda kwa pamoja mwelekeo wa kufanya mashauriano na mazungumzo na kulinda amani na utulivu wa peninsula.

  Kabla ya kufanya mazungumzo, Bw. Xin Jinping amefanya hafla ya kumkaribisha Kim Jong Un kwenye Ukumbi wa kaskazini katika Jumba la mikutano ya umma la Beijing. Baada ya mazungumzo, Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan waliwaandalia tafrija Kim Jong Un na mkewe Ri Sol Ju. Bw. Xi Jinping alipotoa hotuba ya kuwakaribisha, alisema katika majira yajayo ya mchipuko, Kim Jong Un na mkewe wamefanya ziara isiyo rasmi nchini China, ambayo ina umuhimu mkubwa sana kwa ajili ya kuzidisha mawasiliano, kuimarisha na kuhimiza ushirikiano, na ziara hii itasukuma mbele uhusiano kati ya vyama viwili na nchi mbili kwenye ngazi mpya katika kipindi kipya cha historia, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuhimiza amani, utulivu, na maendeleo ya kanda hii. Sasa hivi, mimi na kiongozi mkuu Jim Jong Un tulikuwa na mazungumzo kwa unyoofu na urafiki. Amesema China imeona kwa kauli moja kuwa, kurithi na kuenzi urafiki wa jadi kati ya China na Korea ya kaskazini kunalingana na maslahi ya pamoja ya pande zetu mbili, hili ni chaguo la kimkakati la pamoja kwa pande zetu mbili. Bila kujali mabadiliko ya namna gani yatatokea katika hali ya kimataifa na kikanda, pande mbili zitakumbuka barabara wimbi kuu la maendeleo ya dunia na mambo makuu ya uhusiano wa China na Korea kaskazini, China itaimarisha mawasiliano kati ya viongozi wakuu, kuzidisha mawasiliano ya kimkakati, kupanua maingiliano na ushirikiano ili kuleta manufaa kwa wananchi wa nchi zetu mbili na wa nchi mbalimbali duniani.

  Bw. Kim Jong Un alipotoa hotuba alisema katika hali ambayomambo makubwa hayakutokea hapo kabla katika hali ya Peninsula ya Korea, ana matumaini ya kuhimiza amani na utulivu, kurithi na kuendeleza urafiki kati ya Korea kaskazini na China, na amefanya ziara nchini China. Ziara yake ni yaa mara ya kwanza nje ya nchi, na amekuja nchini China, hii imeonesha nia ya kurithi urafiki wa jadi na kuthamini urafiki kati ya Korea kaskazini na China. Amefanya mazungumzo yenye mafanikio na Rais Xi Jinping kuhusu kuendeleza uhusiano kati ya vyama viwili na nchi mbili, kuhusu hali ya nchini ya kila upande, na kulinda amani na utulivu wa Peninsula ya Korea. Nina imani kuwa, katika majira ya mchipuko yaliyojaa furaha na matumaini, mkutano wa mara ya kwanza kati yangu na katibu mkuu Xi Jinping utaleta matunda kemkem ya urafiki kati ya Korea ya kaskazini na China na kuhimiza amani na utulivu wa Peninsula ya Korea.

  Katika wakati wa ziara yake hii, Bw. Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan waliwaandalia karamu ya mchana Kim Jong Un na mkewe kwenye Ukumbi wa Yangyuanzhai katika Jumba la kuwapokea wageni waheshimiwa wa taifa la Diaoyutai. Xin Jinping amesema, Jumba la kuwapokea wageni waheshimiwa wa taifa la Diaoyutai limeshuhudia maendeleo ya urafiki wa jadi kati ya China na Korea ya kaskazini, viongozi wazee wa vyama viwili na nchi mbili zetu walikuwa na uhusiano mzuri wa karibu umekuwa mfano wetu wa kuigwa. Wamewakaribisha kiongozi mkuu Kim Jong Un na mkewe kuja China mara kwa mara.

  Kim Jong Un amesema, urafiki kati ya Korea kaskazini na China ni wenye thamani kubwa sana. Amesema anapenda kuungana na Rais Xi katika kufuata nia tukufu ya viongozi wazee, kurithi na kuendeleza uhusiano wa kirafiki unaodumisha hali yake ya awali ingawa imepita upepo mkubwa na mvua kubwa, na unahimizwa kuendelezwa kwenye kiwango kipya katika hali mpya ya hivi sasa.

  Kim Jong Un pia ametembelea Maonesho ya matunda mapya ya uvumbuzi ya Taasisi ya Sayansi ya China tokea Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha kikomunisti cha China, ambapo alisifu mafanikio yaliyopatikana nchini China katika maendeleo ya teknolojia na kazi za kufanya uvumbuzi, na aliandika maneno ya kumbukumbu kwa matembezi yake kwenye maonesho hayo.

  Wajumbe wa Ofisi ya siasa wa Kamati kuu ya Chama na viongozi wengine wanaohusika wa China wameshiriki kwenye shughuli husika.

  Viongozi wengine husika wa Kamati kuu ya Chama cha Leba cha Korea ya kaskazini walimfuatana na Kim Jong Un katika ziara yake nchini China na kushiriki kwenye shughuli husika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako