• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Palestina azilaani Marekani na Israel kuzuia mchakato wa amani wa Palestina na Israel

    (GMT+08:00) 2018-03-28 09:49:46

    Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesema mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel umekwamishwa kutokana na vizuizi vinavyowekwa na Marekani na Israel.

    Rais Abbas amesema, msimamo usio wa haki wa Marekani kuhusu hadhi ya Jerusalemu na mashambulizi ovyo ya Israel dhidi ya Palestina yamekwamisha mchakato huo.

    Rais Abbas ametoa wito wa kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu suala hilo ili kuanzisha utaratibu wa kimataifa wa kutatua mgogoro kati yao na kuwasaidia wapalestina kujenga nchi huru yenye mipaka iliyoamuliwa mwaka 1967, na Jerusalem mashariki kuwa mji mkuu wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako