• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masumbwi, Bondia AJ asisitiza kuwa analipa umuhimu pambano la jumamosi, wala hatomdharau mpinzani wake

    (GMT+08:00) 2018-03-28 10:43:08

    Bondia Anthony Joshua AJ wa Uingereza, jana amewaambia waandishi wa habari kuwa, hamuogopi mpinzani wake katika pambano la jumamosi, Joseph Parker wa New Zealand, isipokuwa nia ya mpinzani huyo kuwa na nia ya ushindi ndicho inamfanya asilidharau pambano hilo.

    AJ amesema anataka kuudhihirishia ulimwengu kuwa, licha ya kuwa yeye ni bondia bora, amefanya maandalizi makali kwa ajili ya jumamosi, na hatarajii kuwa pambano litakuwa jepesi.

    Alipoulizwa maoni yake kuhusu pambano jingine dhidi ya bingwa mwingine wa marakani, Deontay Wilder, ili kuthibitisha kuwa akili ameielekeza jumamosi, amesema suala hilo litakuja baada ya pambano kukamilika.

    Katika siku za hivi karibuni, habari zimeendelea kusambaa kuwa Wilder ametangaza nia ya kupigana na yeyote atakayeibuka mshindi katika pambano la jumamosi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako