• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya teknolojia katika soka: Timu ya taifa ya Uingereza yalazimishwa sare ya goli 1-1 na Italia

    (GMT+08:00) 2018-03-28 10:43:35

    Matumizi ya teknolojia katika soka yaliyoasisiwa na FIFA, yamezuia furaha ya timu ya taifa ya Uingereza ambayo ilishindwa kuondoka na ushindi dhidi ya Italia kwenye mechi ya kirafiki, baada ya mwamuzi wa ziada kubaini faulo iliyobainika kupitia msaada wa picha za video.

    Zikiwa zimesalia dakika tatu mpira umalizike, mwamuzi wa video Deniz Ayitekin, alitumia ushahidi wa picha kuwa beki wa Uingereza James Tarkowski alimchezea rafu mchezaji wa Italia, Federico Chiessa katika eneo la hatari, jambo lililosababisha penati iliyopigwa na kuipatia italia goli muhimu lililokuwa la kusawazisha.

    Uamuzi wa video, ulizusha malalamiko kutoka kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza ambao kwa muda mrefu walimzonga mwamuzi.

    Hadi mwisho wa mechi hiyo matokeo yalikuwa sare ya magoli 1-1 kwa kuwa Uingereza walikuwa tayari wanaongoza kwa goli moja lililofungwa na Jamie Vardy kunako dakika ya 26.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako