• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washauri wa usalama wa Marekani, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu wakutana kuhusu suala la Iran

    (GMT+08:00) 2018-03-28 15:07:47

    Washauri wa usalama wa taifa kutoka Marekani, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wamekutana katika ikulu ya Marekani ili kujadili jitihada za pamoja katika kukabiliana na athari mbaya za Iran na vitendo vyake vya uchokozi.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani imesema, maafisa usalama kutoka nchi hizo tatu wamejadili maswala yenye umuhimu wa kimkakati kwa nchi hizo tatu, na wamekubaliana kukutana mara kwa mara ili kuendeleza na kutekeleza mifumo ya pamoja ya kupunguza vitisho dhidi ya usalama wa kikanda na kuleta amani, utulivu na ustawi katika kanda ya Mashariki ya Kati.

    Wakati huohuo, msemaji wa jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia Kanali Turki al-Malki amesema watalipiza kisasi dhidi ya Iran kutokana na nchi hiyo kutoa makombora kwa wapiganaji wa Houthi wa Yemeni kushambulia Saudi Arabia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako