• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufaransa inapenda kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-03-28 15:17:46

    Ufaransa imesema inataka vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya Zimbabwe viondolewe, na serikali mpya ya nchi hiyo ipatiwe misaada na taasisi mbalimbali za kifedha ili kujenga uchumi wake.

    Waziri wa Nchi katika Wizara ya Masuala ya Kigeni na Ulaya Jean-Baptiste Lemoyne ambaye alionana na rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe mjini Abidjan, Cote d'Ivore, amesema Ufaransa inataka kuisaidia Zimbabwe kutekeleza mageuzi yatakayowezesha kuondokana na vikwazo hivyo.

    Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya Zimbabwe miongo miwili iliyopita kufuatia kutoelewana kati ya Zimbabwe na Uingereza juu ya mageuzi ya ardhi ambapo wazungu walinyang'anywa mashamba yao na kugawiwa kwa watu weusi wasiokuwa na ardhi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako