• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mombasa-Wamiliki wa hoteli watarajia wageni wengi wakati wa likizo ya pasaka

    (GMT+08:00) 2018-03-28 19:34:29

    Wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli katika eneo la Pwani nchini Kenya wanatarajia kuongezeka kwa biashara wakati wa likizo ya pasaka.

    Kwa kawaida idadi kubwa ya wageni hutembelea hoteli za fuo za bahari wakati wa kuadhimisha sikukuu ya pasaka.

    Tayari baadhi ya hoteli za pwani ya kusini zimesajili asilimia kubwa ya wageni ambao wengi wao ni watalii kutoka nchini Rwanda,Uganda,na Tanzania.

    Afisa Msimamizi wa Chama cha Wafanyabiashara na Wasimamizi wa Hoteli tawi la Pwani (KAHC) Sam Ikwaye pamoja na Mwenyekiti wa Shirika la Utalii (KTF) Mohamed Hersi walisema wenye hoteli wamewekeza zaidi wakitumai biashara itaongezeka.

    Hersi alisema Pasaka imefika mapema sana wakati huu badala ya Aprili.Alisema kwa kawaida wakenya huwa watu dakika za mwisho,na hivyo wanatarajia hoteli zote zitajaa wageni.

    Kw aupande wake Bw Ikwaye alisema kuimarika kwa biashara kumetokana na kampeni kabambe za kuitangaza pwani kama kivutio cha utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako