• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Unilever Tea kuanza kutumia nishati isiyoharibu mazingira

    (GMT+08:00) 2018-03-28 19:36:27

    Kampuni za Unilever Tea Kenya na Crossboundary Energy zimetia saini mkataba wa kujenga kiwanda cha kutumia nishati ya miale ya jua katika kiwanda chake cha majani chai mjini Kericho.

    Ujenzi wa kiwanda hicho umefadhiliwa na CrossBoundary Energy ambayo imetoa kandarasi kwa kampuni ya SolarCentury East Africa ,kuhusiana na masuala ya kiufundi ya mradi huo.

    Mradi huo unatarajiwa kuanza kutumika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

    Hatua hiyo inalenga kupunguzia kampuni ya Unilever gharama yake ya nishati pamoja na kupunguza kiwango cha kaboni inayotolewa hewani kwa zaidi ya tani 10,000.

    Meneja Mkurugenzi wa Unilever Tea Nicholas Yiannakis amesema mkataba huo unasaidia Unilever kukaribia mpango wake wa kutumia nishati isiyochafua mazingira kwa asilimia 100 kufikia mwaka 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako