• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wafanyabaishara wadogo waingizwa kwenye mfumo wa ulipaji kodi

    (GMT+08:00) 2018-03-28 19:36:55

    Wafanyabiashara wadogo wasio kwenye sekta rasmi wameanza kupatiwa vitambulisho maalum ili kuingizwa kwenye mfumo wa ulipaji kodi.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana jijjini Dar es Salaam,Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ,TRA,Charles Kichere,wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga,alisema kwa wafanyabiashara hao watakuwa wanalipia Sh10,000 kama gharama ya kuchangia kitambulisho hicho.

    Alisea utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara hao unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge la Bajeti la mwaka 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabishara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako