• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Wadau sekta ya utalii Rwanda wapongeza Afrika Kusini kuondoa vikwazo vya visa

    (GMT+08:00) 2018-03-28 19:37:19

    Wadau katika sekta ya utalii nchini Rwanda wamepongeza mapendekezo ya Afrika Kusini ya kuwaondolea wanyarwanda vikwazo vya visa,wakisema hatua hiyo hiyo itapiga jeki shughuli zao na kuongeza idadi ya watalii.

    Rais mpya wa Afrika Kusini alitangaza uamuzi huo wakati wa mkutano wa kilele Umoja wa Afrika jijini Kigali wiki iliyopita.

    Afisa wa kampuni ya utalii ya Wlidlife Tours,Davidson Mugisha amesema kampuni zinazoendesha shughuli za utalii kwa muda mrefu zimeshindwa kuitangaza Rwanda vizuri Afrika Kusini kutokana na vikwazo vya visa.

    Alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya watalii kutoka Afrika Kusini kwa sababu raia wa Afrika kusini wana utamaduni wa kutalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako