• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Lubenga ahimiza fursa za uchumi wa viwanda

    (GMT+08:00) 2018-03-28 19:37:39
    Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Ngemela Lubinga,amewataka wananchi wilayani Momba mkoani Songwe kuchangamkia fursa za viwanda ili kujikwamua na umaskini kwa kuwa kaulimbiu ya serikali ya sasa ni uchumi na viwanda.

    Alitoa kauli hiyo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha chumvi kilichopo kata ya Ivuna ambapo alisema mradi huo ukitumiwa vizuri utainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na serikali kwa ujumla.

    Lubinga alishauri wanufaika wa mfuko wa Jamii (TASAF) washirikishwe katika uchumi wa viwanda ili waweze kujikwamua kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako