• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yatoa wito kwa wananchi kujitokeza kupiga kura

    (GMT+08:00) 2018-03-29 09:08:47

    Serikali ya Misri imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura zao katika siku ya mwisho ya upigaji kura wa uchaguzi mkuu, wakati rais wa sasa Abdel Fattah al-Sisi anatarajiwa kushinda muhula wa pili wa kipindi cha miaka minne. Maofisa wa serikali na majaji wamewataka raia wa Misri kujitokeza kupiga kura zao, ikiwa ni wajibu wao wa kitaifa wa kuunga mkono uongozi wa sasa kwa ajili ya usalama, utulivu na maendeleo katika siku zijazo. Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Misri, watu milioni 60 kati ya wote milioni 104 wa nchi hiyo wanastahiki kupiga kura kwenye vituo zaidi ya elfu 13 kote nchini Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako