Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amesema hatua za upande mmoja zinaweza kuwa ni tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia.
Akiongea kwenye mjadala wa njia ya simu wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hatua za pamoja za kuimarisha operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, Bw. Mahamat amesema kila juhudi zinapaswa kufanywa kulinda utaratibu wa pande nyingi.
Amesema operesheni za kulinda amani zilizoidhinishwa na Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ni msingi wa juhudi za kimataifa za kuhimiza amani na usalama, ambazo zinaonesha umuhimu wa utaratibu wa pande nyingi na mshikamano wa dunia nzima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |