• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Sudan arefusha muda wa usitishaji vita kwa miezi mitatu zaidi

    (GMT+08:00) 2018-03-29 09:38:38

    Shirika la habari la Sudan SUNA limeripoti kuwa Rais Omar al-Bashir wa Sudan ametoa agizo la kurefusha muda wa usitishaji vita kwa miezi mitatu zaidi kwenye maeneo yote yenye mapambano nchini humo.

    Ripoti imesema rais Omar al-Bashir ametoa agizo la kurefusha muda wa kusimamisha vita hadi tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

    Katika miaka ya hivi karibuni serikali ya Sudan na makundi ya upinzani yenye silaha wamekuwa wakifanya juhudi za kurefusha muda wa usitishaji vita katika maeneo yenye mapambano. Mwezi Juni mwaka 2016, rais al-Bashir alitangaza kusimamisha vita kwa muda wa miezi minne, ili kuwapatia waasi nafasi ya kujiunga na mazungumzo ya kitaifa, na baadaye akarefusha muda wa kusimamisha mapambano kwa mara kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako