• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNMISS yaanzisha kampeni ya kulinda usalama barabarani Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:04:43

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS imeanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo inatoa vifaa vya usalama kwa mamia ya watumia pikipiki kwa ajili ya biashara ili kuzuia ajali barabarani.

    Mkuu wa UNMISS David Shearer amesema biashara ya usafiri wa pikipiki, ambayo ni njia ya kawaida ya usafiri mjini Juba na katika miji ya jirani nchini Sudan Kusini, ni muhimu kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Bw. Shearer ameeleza kuwa familia nyingi zinategemea biashara hiyo kujikimu kimaisha, wakati nchi hiyo inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako