• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kriketi, Uganda: Timu ya taifa yaendelea kuimarishwa kwa ajili ya mashindano ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-03-29 10:31:19

    Chama cha mchezo wa Kriketi nchini Uganda UCA kimesema tangu timu ya taifa ishushwe daraja katika viwango vya ubora na kiushindani na baraza la Kimataifa la mchezo wa Kriketi ICC, kamwe hakijalala isipokuwa kimeendelea kuimarisha timu ya taifa ili kiweze kupandishwa tena daraja.

    Katika kuthibisha hilo, timu ya taifa ya Uganda imesafiri kwa ajili ya michezo ya kirafiki kwenye nchi za Rwanda, Qatar na India.

    Pia timu hiyo inatarajiwa kucheza na Saudi Arabia katika siku za hivi karibuni kabla ya kusafiri kwenda Malaysia April 28.

    Kocha mkuu wa timu ya taifa, Steve Tikolo amesema wachezaji, uongozi wa timu ya taifa pamoja na UCA, wanafanya juhudi za pamoja ili kuhakikisha wanarejesha hadhi ya Uganda katika Kriketi ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako