• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haikubali kulazimishwa kufanya mazungumzo kufuatia mgogoro wa kibiashara kati yake na Marekani

    (GMT+08:00) 2018-03-29 16:28:29

    China haikubali kulazimishwa kufanya mazungumzo kuhusiana na mgogoro wa kibiashara uliopo kati yake na Marekani.

    Hayo yamesemwa na msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Gao Feng leo hapo Beijing kutokana na habari zinazosema kuwa China na Marekani zinafanya mazungumzo ili kuepusha vita ya biashara kati yao, na huenda nchi hizo mbili zitaacha kuongezana ushuru dhidi ya bidhaa zao.

    Bw. Gao amesisitiza kuwa mazungumzo yanatakiwa kufanywa katika hali ya usawa. Anasema, "China iko tayari kufanya mazungumzo, lakini kuna masharti. Marekani inatakiwa kuacha sera ya upande mmoja na vitendo vya kujilinda kibiashara. Mazungumzo yanatakiwa kufanywa katika hali ya usawa, na China haitalazimishwa na upande mmoja kufanya mazungumzo hayo. Pia mazungumzo yanatakiwa kuwa ya kiujenzi, kuwa na uwiano, mambo hayo yanahitaji juhudi za pamoja."

    Mwakilishi wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer jana alisema nchi hizo mbili zinatarajiwa kufanya mazungumzo ambayo yanaweza kuleta matokeo mazuri. Pia amesema Marekani itaongeza muda wa kutangaza orodha ya bidhaa za China zitakazoongezewa ushuru kwa umma kutoka siku 30 hadi 60, ikimaanisha kuwa katika siku chache zijazo serikali ya Marekani haitaongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako