• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mpya wa ulinzi wa China kufanya ziara ya kwanza nchini Russia

    (GMT+08:00) 2018-03-29 19:29:16

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China kanali Ren Guoqiang amesema, kuanzia tarehe 1 hadi 8 mwezi ujao, mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri mpya wa ulinzi wa China Jenerali Wei Fenghe atahudhuria mkutano wa 7 wa usalama wa kimataifa wa Moscow na kufanya ziara nchini Russia na Belarus.

    Akizungumzia sababu ya Jenerali Wei kufanya ziara yake ya kwanza nchini Russia baada ya kuteuliwa kuwa waziri mpya wa ulinzi wa China, Kanali Ren amesema uhusiano kati ya China na Russia ni wenzi wakuu na muhimu wa uratibu wa kimkakati, na uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni uhusiano unaoendelezwa vizuri zaidi kati ya nchi kubwa duniani. Ameongeza kuwa miaka ya hivi karibuni, chini ya uhimizaji wa rais Xi Jinping wa China na mwenzake Vladimir Putin wa Russia, uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili uko katika kiwango cha juu, huku ushirkiano kati yao ukiimarishwa na maelewano yakiongezeka. Ziara ya Jenerali Wei ni hatua ya kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, na itasaidia kuzidisha ushirkiano wenye ufanisi kati ya majeshi hayo mawili na kuzidi kuendeleza uhusiano wa kiwenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako