• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania na Uturuki kushirikiana katika sekta ya utalii

    (GMT+08:00) 2018-03-29 19:48:47

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameihakikishia Uturuki kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya pande mbili hizo na kusisitiza ushirikiano katika sekta ya utalii kati ya Zanzibar na mji wa kitalii wa Antalya nchini humo.

    Alisema hayo jana wakati alipozungumza na Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutaglu aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kujitambulisha na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar.

    Katika mazungumzo hayo, Rais Shein alimueleza Balozi huyo kuwa uchumi wa Zanzibar unategemea kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii, hivyo ni vyema ushirikiano uimarishwe zaidi kwa watalii wanaofika eneo la kitalii la Antalya nchini Uturuki wakafika na Zanzibar.

    Alieleza kuwa mji wa kitalii wa Antalya nchini Uturuki, umebarikiwa kuwa na vivutio vingi sambamba na hali ya hewa nzuri, ambapo sifa zote hizo zinafanana na Zanzibar, hivyo ni vyema ukawepo ushirikiano kati ya pande mbili hizo katika kuwashawishi watalii wanaofika Antalya kufika pia Zanzibar.

    Rais Shein alieleza kuwa changamoto ya usafiri wa moja kwa moja kati ya Uturuki na Zanzibar iliyokuwepo siku za nyuma, hivi sasa haipo kutokana na kuwepo kwa usafiri wa ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki inayofanya safari zake kati ya Istanbul na Zanzibar.

    Shein pia alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi huyo wa Uturuki, fursa iliyotolewa na Zanzibar kwa kuikaribisha nchi hiyo kuweka ubalozi wake mdogo hapa Zanzibar, kama ilivyo kwa baadhi ya nchi kama vile, China, India, Msumbiji na Misri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako