• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuelekea Kombe la Dunia: FIFA yateua waamuzi (marefarii) wawili kutoka Kenya na Burundi kwa ajili ya mashindano ya kombe la Dunia.

  (GMT+08:00) 2018-03-30 08:35:43

  Waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu kutoka Kenya Aden Range Marwa, na Jean Claude Birumushahu wameorodheshwa kuwa waamuzi wasaidizi katika mashindano ya kombe la dunia yanayoanza mwezi juni nchini Urusi.

  Kutokana na uteuzi huo uliofanywa na FIFA, Marwa na Jean Claude watashirikiana na waamuzi wasaidizi wengine 61 pamoja na waamuzi wa kati 36.

  Tangu uteuzi huo ufanyike jana, waamuze wote 90 wakiwemo Marwa na Jean Claude, watakuwa chini ya uangalizi na udhamini wa FIFA kuanzia majukumu yao kwenye nchi zao mpaka watakapokuwa kwenye kombe la dunia, na katikati ya mwezi April watakwenda Italia kwa ajili ya semina elekezi.

  Waamuzi wengine kutoka Afrika ni wa nchi za Morocco, Africa Kusini, Sudan, Senegal, Angola, Algeria, Tunisia na Zambia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako