• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbio za Baiskeli, Rwanda: Bayingana abaki kuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa Shirikisho katika uchaguzi utakaofanyika jumamosi

    (GMT+08:00) 2018-03-30 08:37:08

    Aimable Bayingana ameendelea kuwa mgombea pekee wa kiti cha Urais wa Shrikisho la mchezo wa mbio za baiskeli nchini Rwanda FERWACY baada ya watu kutojitokeza kugombea nafasi hiyo.

    Uchaguzi mkuu wa FERWACY unafanyika jumamosi hii, na kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati inayosimamia uchaguzi huo, nafasi zingine pia zimepata mgombea mmoja kila moja.

    Wachambuzi wa masuala ya Baiskeli nchini Rwanda wamedai, uongozi bora na maendeleo ya mchezo huo tangu Bayingana achukue wadhifa huo vimepatikana na ndiyo maana wadau, na mashabiki wa mchezo huo wanaunga mkono jitihada zake.

    Bayingana amekuwa Rais wa FERWACY tangu mwaka 2010 na mwaka jana ameteuliwa tena kuwa mjumbe wa bodi ya maendeleo ya mchezo wa mbio za baiskeli Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako