• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi kazi cha Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa kuwasaidia wahamiaji waliokwama Libya

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:02:54

    Kikosi kazi cha pamoja cha Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa kinafanya juhudi za kuwasaidia wahamiaji wa nchi za Afrika waliokwama nchini Libya, na kufanya juhudi za kuvunja mitandao inayofanya magendo ya binadamu na usafirishaji wa wahamiaji.

    Kwenye mkutano wa kikosi kazi hicho uliofungwa jana mjini Addis Ababa, kamishna wa mambo ya kijamii wa Umoja wa Afrika Bi. Amira Elfadil, amesema hali ya wahamiaji kwenye maeneo yanayodhibitiwa na serikali imeboreshwa. Hata hivyo amesema hali ya wakimbizi nchini Libya inahitaji ufuatiliaji mkubwa, kwa kuwa kuna wahamiaji wengine kwenye maeneo yanayodhibitiwa na makundi yenye silaha na vituo binafsi.

    Amesema mpaka sasa amefanikiwa kuwasaidia wahamiaji elfu 16, na 1,000 kati yao walipelekwa Niger kwa ajili ya kupelekwa katika nchi ya tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako