• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa umoja wa mataifa asema mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio kwa binadamu

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:03:14

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres amesema mabadiliko ya hali ya hewa ni tishio kwa binadamu kuliko wakati wowote ule.

    Bw. Guterres amezikumbusha serikali na jamii kuhusu tishio hilo na kasi yake, ambayo inaweza kuzidisha uwezo wa kukabiliana nayo. Amesema tayari mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta madhara kwa binadamu katika dunia nzima, na hatua zinatakiwa kuchukuliwa katika muda mfupi na mrefu kukabiliana na tatizo hilo.

    Amesema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, mwaka jana mabadiliko ya hali ya hewa yalisababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni 320, watu milioni 41 katika nchi za Asia kusini na laki 9 wa Afrika waliathiriwa na mafuriko.

    Bw. Guterres amesema dunia inatakiwa kupunguza utoaji wa hewa chafu kwa asilimia 25 kabla ya mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako