• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN-Habitat yaahidi kukabiliana na changamoto zinazotokana na kukua kwa miji

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:03:31

    Mkuu mpya wa Shirika la mpango wa makazi la Umoja wa mataifa UN-Habitat Bibi Maimunah Sharif amesema shirika hilo litatoa kipaumbele kuhimiza upatikanaji wa nyumba ili kukabiliana kwa ufanisi na changamoto za ukuaji wa kasi wa miji.

    Bibi Shariff amesema kwa sasa UN Habitat inaongozwa na kanuni ya ajenda mpya kuhusu miji na malengo ya maendeleo endelevu kwenye kukabiliana na changamoto za kukua kwa miji.

    Ajenda mpya kuhusu miji ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa UN-Habitat mwaka 2016, yanayolenga kuongoza juhudi za ukuaji wa miji kati ya nchi, miji na viongozi wa kikanda, wafadhili wa kimataifa, mipango ya umoja wa mataifa na jumuiya za kiraia kwa miaka 20 ijayo.

    Bibi Sharif amesema kama ukuaji wa miji ukipangwa vizuri utasaidia kufanikisha utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako