• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yajitahidi kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:18:25

    Kenya imeimarisha mfumo wake wa uwekezaji na wa sheria ili kuvutia uwekezaji zaidi kutoka China hasa katika sekta za maendeleo ya viwanda, wakati inatafuta kufikia lengo la kujijenga kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2030.

    Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema wawekezaji binafsi wa China wanatakiwa kutumia fursa inayotolewa na maeneo maalumu ya kiuchumi ambayo yameanza kutoa huduma sasa. Pia amesema Kenya imekamilisha marekebisho ya sheria za uhusiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma, kwa hiyo sasa ina uwezo wa kitaasisi.

    Ameongeza kuwa Kenya ina imani kuwa uhusiano wa kiserikali kati yake na China utaimarika, pia inataka wawekezaji wengi zaidi wa China kuja Kenya kujenga viwanda vya uzalishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako