• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Afrika watahadharishwa kuwa uko hatarini kushambuliwa kimtandao

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:19:30

    Wataalamu wa TEHAMA wametahadharisha kuwa uchumi wa Afrika uko kwenye hatari kubwa ya kushambuliwa kimtandao, kutokana na ukosefu wa utaalamu wa kukabiliana na mashambulizi ya kimtandao.

    Wataalamu waliyasema hayo wanapohudhuria mkutano wa kilele wa Cloud and Security mjini Kigali, Rwanda, ambao unafuatilia umuhimu wa usalama wa mtandao katika uvumbuzi wa kibiashara kwenye kanda hiyo.

    Mhandisi mkuu wa usalama wa Afrika Mashariki wa kampuni ya Check Point Software Technologies Bw. Michael Tumusiime, amesema wakati watu wengi wanazidi kutumia internet, serikali na makampuni zikiongeza matumizi ya internet, bado hakuna ujuzi wa kitaaluma wa kutosha kulinda data za serikali na makampuni dhidi ya mashambulizi ya kimtandao. Ameongeza kuwa nchi nyingi za Afrika zimefanya juhudi kukabiliana na uhalifu wa kimtandao, lakini baadhi hazina bajeti na mafunzo ya kuwaandaa wataalamu wa usalama wa mtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako