• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yatoa wito wa madaraka kugawanywa katikati mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-03-30 09:24:46

    Jumuiya ya maendeleo ya kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD imetoa wito kwa makundi yanayopambana katikati mwa Somalia yatekeleze mpango wa ugawanyaji wa madaraka ulio shirikishi, baada ya kufikia makubaliano mwaka jana.

    IGAD imesema imeanza kutekeleza makubaliano ya amani yaliyosainiwa kati ya serikali ya Galmudug na kundi la ASWJ mwezi Desemba mwaka jana, yenye lengo la kuziunganisha pande mbili zilizotengana ili kuwa chini ya utawala mmoja.

    IGAD imesema pande mbili zimeunganisha mabunge yao na kukubaliana kuwagawa nafasi za wabunge kwa koo mbalimbali, baada ya mazungumzo ya kisiasa. Makundi hayo mawili yamekubali kuunga mkono amani na kufuata makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako